Psalms 118

Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi


1 aMshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.


2 bIsraeli na aseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”

3 cNyumba ya Haruni na iseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”

4 dWote wamchao Bwana na waseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”


5 eWakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,
naye akanijibu kwa kuniweka huru.

6 f Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa.
Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

7 g Bwana yuko pamoja nami,
yeye ni msaidizi wangu.
Nitawatazama adui zangu
wakiwa wameshindwa.


8 hNi bora kumkimbilia Bwana
kuliko kumtumainia mwanadamu.

9 iNi bora kumkimbilia Bwana
kuliko kuwatumainia wakuu.


10 jMataifa yote yalinizunguka,
lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

11 kWalinizunguka pande zote,
lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

12 lWalinizunguka kama kundi la nyuki,
lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo;
kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.


13 mNilisukumwa nyuma karibu kuanguka,
lakini Bwana alinisaidia.

14 n Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu,
yeye amefanyika wokovu wangu.


15 oSauti za shangwe na ushindi
zinavuma hemani mwa wenye haki:
“Mkono wa kuume wa Bwana
umetenda mambo makuu!

16 pMkono wa kuume wa Bwana
umeinuliwa juu,
mkono wa kuume wa Bwana
umetenda mambo makuu!”


17 qSitakufa, bali nitaishi,
nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.

18 r Bwana ameniadhibu vikali,
lakini hakuniacha nife.


19 sNifungulie malango ya haki,
nami nitaingia na kumshukuru Bwana.

20 tHili ni lango la Bwana
ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.

21 uNitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu,
umekuwa wokovu wangu.


22 vJiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni.

23 w Bwana ametenda hili,
nalo ni la kushangaza machoni petu.

24 xHii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,
tushangilie na kufurahi ndani yake.


25 yEe Bwana, tuokoe,
Ee Bwana, utujalie mafanikio.

26 zHeri yule ajaye kwa jina la Bwana.
Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.

27 aa Bwana ndiye Mungu,
naye ametuangazia nuru yake.
Mkiwa na matawi mkononi,
unganeni kwenye maandamano ya sikukuu
hadi kwenye pembe za madhabahu.


28 abWewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,
wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.


29 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.
Copyright information for SwhKC